WABRAZIL WAPAGAWISHWA NA NGOMA ZA KIHINDI TAMASHA LA BRAZILIAN CARNIVAL

MASHABIKI wa burudani nchi Brazil wamepagawishwa na ngoma za Kihindi ambazo zinatesa kwa mara ya kwanza, kwenye tamasha la kila mwaka la “The Brazilian Carnival”.

Kwa mara ya kwanza tamasha hilo ambalo linahusisha burudani mwanzo mwisho, limeshirikisha wasanii kutoka Bollywood ambao wamealikwa kutumbuiza.

Imeelezwa kuwa sababu ya kualikwa kwa wasanii hao ni kutokana na maombi ya mashabiki wenyeji wa Amerika Kaskazini ambao ni Wahindi wekundu, lakini ujio wake umewakuna wote.


Picha zilizosambazwa zinazowaonyesha wasanii hao kutoka India wakiwa wamevalia mavazi ya kiasili huku wakipagawisha kwa kucheza, zimesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.

No comments