WAFUNGAJI WA MAGOLI YOTE YA MANCHESTER UNITED MSIMU HUU … Ibrahimovic hana mpinzani


Hakuna ubishi kuwa kwa sasa mshambuliaji mkongwe Zlatan Ibrahimovic ndiye roho ya Manchester United.

Ibrahimovic ameifungia Manchester United mabao 26 katika michuano yote huku anayefuatia Juan Mata akiachwa mbali kwa mabao yake tisa.

Anthony Martial,  na kiungo Paul Pobga ndio wanaofuatia kwa kufunga magoli saba kila mmoja wakati Henrikh Mkhitaryan anashika namba nne kwa bao zake sita akimpita Wayne Rooney kwa goli moja.

Jesse Lingard amefunga mara nne, Marouane Fellaini na Chris Smalling kila mmoja ana magoli mawili huku Daley Blind, Michael Carrick, Ander Herrera na Bastian Schweinsteiger wameambulia goli moja kila mmoja.

Zlatan Ibrahimovic 
No comments