WAGOSI WA KAYA WABISHA HODI KWENYE GEMU KWA MARA YA PILI

UWEZEKANO wa kundi lililotikisa sana lilipoundwa miaka ya 2000, “Wagosi wa Kaya” kutoka Tanga kurejea tena ni mkubwa.

Hayo yamebainishwa na mmoja wa wakali waliokuwa wakiunda kundi hilo, Fred Maliki maarufu kama “Mkoloni” ambaye amesema wanajipanga kufanya kazi za kundi mwaka huu.

Mkoloni ambaye kwa kushirikiana na mwenzake Dk. John walitingisha sana anga za muziki wa kizazi kipya nchini kutokana na staili ya uimbaji wao, alisema kuna mambo mengi wamepania kuyafanya.

“Kuna kazi ambazo tunajipanga kuzifanya kama kundi la Wagosi wa Kaya, tunajua mashabiki wetu wametumiss sana lakini tulilazimishwa na michakato ya kimaisha na sasa tunawaambia muda si mrefu wataziona kazi zetu,” alisema Mkoloni.

No comments