WENGER ASEMA SANCHEZ ATAONDOKA ARSENAL KWA UTASHI WA KLABU


Arsene Wenger amesisitiza kuwa Arsenal ndiyo itakayoamua hatma ya Alexis Sanchez na sio utashi wa wa mchezaji. 

Pamoja na hayo Wenger ameweka wazi kuwa hana bifu lolote na mshambuliaji huyo na kwamba sababu ya kumwanzisha benchi katika mchezo dhidi ya Liverpool, zilikuwa za kimbinu zaidi.

Wenger akawaambia waandishi wa habari: "Nilishawaambia tangu baada ya mchezo kuwa zilikuwa ni sababu za kiufundi. Najua mnapenda kujaza magazeti yenu."

No comments