Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger yuko lawamani baada timu yake kukubali kichapo cha aibu cha bao 3-1 kutoka kwa Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal waliosafiri kwenda Anfield wakanyanyua mabango yaliyoashiria kumchoka kwao Wenger. Moja ya bango lilindikwa "Ondoka Wenger".

Kocha huyo pia hakueleweka kwa kumwazisha benchi mshambuliaji tegemeo Alexis Sanchez ambaye alisugua benchi hadi mwanzoni mwa kipindi cha pili lakini wakati huo tayari Arsenal ikiwa nyuma 2-0.

Kwa matokeo hayo, Arsenal imeporomoka hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu huku Liverpool ikikwea hadi nafasi ya tatu.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac