WENGER SASA ASHAURIWA KUMSAJILI MKONGWE JOHN TERRY

WENYE Arsenal wao hawafurahishi hata kidogo na mambo yanavyokwenda katika klabu hiyo na wengine wamekuwa wakitoa ushauri mbalimbali.

Mtu mmoja tu anatupiwa mzigo wa lawama zote. Huyu ni kocha Arsene Wenger ambaye ndie mwenye dhamana ya kuamua matokeo ya klabu yake.

Mmoja wa watu nguli katika soka la Uingereza, Harry Redknapp amesikitishwa na mwenendo wa timu na amesema kwamba kuna utoto mwingi hasa katika safu ya ulinzi.

Harry amesema kwamba anaitazama Arsenal ya sasa na ile ambayo anaijua siku nyingi, anaona kwamba kocha Wenger anatakiwa kufanya maamuzi makubwa kama anataka kuendelea kuwashawishi mashabiki wa Arsenal dunia nzima kwamba anafaa kuendelea kuinoa timu hiyo.

Amesema kwamba, kama angekuwa yeye ndio Wenger, chaguo lake la kwanza katika safu za ulinzi angekuwa mkongwe John Terry.

Redknapp anaamini kwamba kukosekana kwa uongozi katika uwanja kumeisumbua sana timu hiyo na mtu sahihi anayemuona kwamba anaweza kuongoza wenzake ni nahodha wa Chelsea, john Terry.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza hana namba katika kikosi cha sasa cha kocha wa Chelsea, Antonio Conte na amedaiwa amefunguliwa milango ya kujiunga na timu nyingine mkataba wake ukikoma.

Akizungumza katika kipindi cha Alan Brazil Sports Breakfast, kocha huyo wa zamani wa Totthen Ham na QPR amesema kwamba kama angekuwa Wenger hata kesho angemsajili Terry.

Kuna mambo anayoona kwamba hayaendi, utoto umezidi na anaona kama hakuna kiongozi uwanjani.

“Kwangu mimi naona kama Terry angeibeba sana Arsenal ingawa sio lazima ushauri wangu usikilizwe,” amesema.

No comments