YANGA SC, PRISONS YA MBEYA KUMINYANA APRILI 22 UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM

YANGA SC itaminyana na Prisons ya Mbeya Aprili 22, mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika robo fainali ya mwisho ya Kombe Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Taarifa kutoka TFF zimesema kwamba michezo miwili ya mwisho ya Robo Fainali za ASFC zimepangiwa tarehe tarehe na pazia la nane bora litafungwa Aprili 22.

Mbali na mchezo kati ya Yanga na Prisons, Azam FC wataikaribisha Ndanda FC ya Mtwara Aprili 5, mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Tayari Simba ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza zimekwisha fuzu hatua  ya Nusu Fainali baada ya kuzitoa Kagera Sugar ya Bukoba na Madsini FC ya Arusha katika Robo Fainali.


Mbao FC iliwafunga Kagera Sugar 2-1 uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati Simba FC iliwafunga Madini FC 1-0 Uwanja wa ShekheAmri Abeid mjini Arusha bao pekee la Mrundi, Laudit Mavugo.

No comments