ZAHIR ALLY ZORRO ASAKA WAFADHILI KUIRUDISHA UPYA MASS MEDIA BAND

MKONGWE wa muziki wa dansi aliyewahi kusumbua na bendi ya Kimulimuli, Zahir Ally Zorro anatafuta mfadhili ili kulirudisha upya kundi lake la Mass Media lililopata kutesa na kibao “Betrice Affair”.

Akipiga stori na Saluti5, Zorro amesema kuwa tayari ameshanunua vyombo vyenye thamani vya zaidi ya mil 40 na wakati wowote, baada ya ufadhili bendi hiyo itarudi upya.

Amesema, hana haraka na kuifufua upya Mass Media, hasa kwa vile anafahamu kwamba mambo mazuri hayataki pupa, hivyo anajipanga polepole huku akitafuta wafadhili wa kumwezesha zaidi kuiendesha bendi hiyo.


“Siwezi kusema lini Mass Media itaibuka rasmi, ila nakimbizana kuona namna nitakavyorejea katika sura ambayo mashabiki watajutia kimya change cha muda mrefu,” amesema.

No comments