ZINEDINE ZIDANE ASEMA ANAHITAJI KUWA MUDA MWINGI DIMBANI ISCO, ALVARO

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa anahitaji kuwapa muda mwingi zaidi wa kucheza nyota wake Isco na Alvaro Morata, baada ya kuisaidia timu hiyo kutoka nyuma na kisha wakafanikiwa kuondoka na ushindi dhidi ya Villareal katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania “La Liga” uliopigwa juzi.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Estadio de la Ceramica, vijana hao wa Zidane walilazimika kutoka nyuma kwa mabao mawili na kisha wakaondoka kifua mbele kwa ushindi wa 3-2, yaliyofungwa katika dakika ya 26 za mwisho.

Isco alitokea benchi wakati matokeo yakiwa 2-0 na akatoa mchango mkubwa uliosaidia kupatikana mabao mawili wakati Morata aliingia uwanjani wakati timu hizo zikiwa 2-2 na kisha akafunga bao la ushindi wakati zikiwa zimebaki dakika saba.

Msimu huu Isco na Morata wamechezeshwa mechi 11 na saba za Ligi na kwa matokeo hayo ya juzi, Zidane amesema kuwa kuna kitu kinatakiwa kufanyiwa mabadiliko.

“Hakuna shaka kwamba Isco na Morata wanahitaji muda zaidi wa kucheza,” kocha huyo wa Real Madrid aliwaambia waandishi wa habari.


“Wamefanya kazi nzuri na kubadili mchezo kwa upande wetu. Nimebaini wanahitajika katika kisi chote,” aliongeza.

No comments