ZLATAN IBRAHIMOVIC HUYOOO LA GALAXY MAREKANI

ZLATAN Ibahimovic amefurahia msimu mzuri katika kikosi cha Manchester United, lakini kuna habari mbaya ambayo wapenzi wa timu hiyo hawataipenda.

Klabu ya La Galaxy ya Marekani imethibitisha juzi kwamba imeongea na Zlatan Ibrahimovic ili kumsajili kutoka Manchester United baada ya kumalizika kwa mkataba wake.


Ibrahimovic ameng’ara sana katika kikosi cha man United huku akiwa amepachika mabao 26 katika mechi zote, lakini inadaiwa kwamba anaweza kuondoka katika klabu hiyo.

No comments