ADHABU YA KUFUNGIWA KWA MANARA NA TFF KWAZUA HOFU KWA WASEMAJI WA TIMU NYINGINE

OFISA Habari wa timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, Masau Bwire amesema Shirikisho la soka Tanzania halitakiwi kukimbilia kuwaadhibu wadau wake, badala yake wangekuwa wanatoa onyo kwanza.

Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Kamati yake ya Maadili kumfungia msemaji wa Simba, Haji Manara, msemaji wa Ruvu Shooting ameibuka na kusema kuwa ameingiwa na hofu kutokana na tukio hilo, lakini akaonya kwamba akionewa au timu yake ikidhulumiwa, hatanyamaza, atasema tu.

Kamati ya maadili ya TFF, imemfungia Manara kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miezi 12 na faini ya sh. mil 9, baada ya kukutwa na makosa matatu ya kinidhamu dhidi ya Shirikisho hilo ikiwa ni kitendo chake cha kuituhumu kutokana na utendaji wake.

Aidha, ukiachana na Manara ambaye amefungiwa wikiendi iliyopita, pia TFF kupitia Kamati yake hiyohiyo ya Maadili, ilimfungia msemaji wa yanga, Jerry Muro kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja Julai, mwaka jana.

Masau amesema kuwa amesikitishwa na hatua 
iliyochukuliwa ya Manara kufungiwa mwaka mmoja na kudai kuwa kitendo hicho kinatia hofu kwa wachezaji wengine.

“Nimesikitishwa na hukumu ya Haji kama binaadamu mwenye roho ya huruma, mkiwa mnafanya kazi pamoja kasha mwenzio akaondolewa haileti picha nzuri, nilihitajhi kupata chalenji kutoka kwake kwani ukiwa na mwenzao wa upande wa pili mkiwa mnajibizana ndipo unapopata akili na kujifunza kunakosababisha kupata ubunifu zaidi.”


“TFF wanatakiwa waangalie sio tu kosa kidogo wanakimbilia kutoa adhabu kubwa na kumfungia mtu, wanatakiwa wawape onyo kwanza, hivyo hali hii inaogopesha watu wengine kuzungumza,” alisema Bwire.

No comments