ALLY CHOCKY YUPO HANDENI PASAKA, TWANGA WAPO GIRAFFE HOTEL …Mkesha Chocky Tanga, Twanga wapo Mango Garden


Bendi ya Twanga Pepeta itakula Pasaka ndani ya hoteli ya kimataifa ya Giraffe, jijini Dar es Salaam, lakini staa wake Ally Chocky atakuwa mjini Handeni.

Chocky atatumbuiza katika onyesho maalum la miaka yake 30 kwenye ‘game’ ya muziki wa dansi, litakalofanyika Makuti Hotel Jumapili Aprili 16.

Wakati Twanga watakuwa Mango Garden Jumamosi ya mkesha wa Pasaka, Chocky siku hiyo atakuwa Tanga mjini katika onyesho litakalofanyika Mkwakwani Stadium akishirikiana na King Kiki, Hamza Kalala na Chaz Baba.

No comments