Habari

ALVARO MORATA WA REAL MADRID AJIPELEKA MWENYEWE CHELSEA

on

Mshambuliaji wa Real Madrid  Alvaro Morata ametamka neno tamu kwenye masikio ya mashabiki wa Chelsea baada ya kukiri kuwa amekuwa akipokea simu kutoka London na kwamba angependa kucheza chini ya kocha Antonio Conte.
Chelsea imekuwa ikitajwa kumwania Morata katika dirisha lijalo la usajili na sasa kauli ya nyota huyo wa Hispania inazidi kuchochea utambi.
Antonio Conte alimsajili Morata ndani Juventus kabla hajaenda kufunidsha timu ya taifa ya Italia huku baadae mshambuliaji huyo akirejea Real Madrid.
Sasa Conte ameonyesha kuhitaji tena huduma ya Morata mwenye umri wa miaka 24 na jambo jema kwake ni kwamba nyota huyo amesema anaamini atacheza tena chini Conte kama si sasa basi ni baadae.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *