ANTHONY MARTIAL NA ROONEY PROVE WATHIBITISHA KUNA MAISHA BILA IBRAHIMOVIC


Anthony Martial na Wayne Rooney wamethibitisha kuwa Manchester United bado ni imara bila Zlatan Ibrahimovic ambaye atakosa msimu mzima uliobakia baada ya kuumia goti.

Washambuliaji hao wawili kila mmoja alifunga bao moja katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa Premier League.

Martial alipokea pasi ndefu ya Paul Pogba kisha akakokota kabla ya kutoa pande kwa Ander Herrera  aliyeuridisha tena kwa  Martial ambaye bila makosa akakwamisha wavuni bao la kwanza kunako dakika ya 21.

Kwa mara nyingine tena, Pogba alianzisha ‘muvu’ iliyozaa bao la pili kwa kumchungulia na kumpelekea pande tamu Martial aliyemsogezea Rooney aliyefunga katika dakika ya 39.

United ipata hofu baada ya Pogba kumia dakika ya 90 na kutolewa nje nafasi yake ikizibwa na Carrick.

Burnley (4-4-2): Heaton 6; Lowton 5, Keane 6, Mee 6 (Tarkowski 46, 5.5), Ward 5.5; Boyd 5.5 (Gudmundsson 62, 6), Hendrick 6, Barton 5, Brady 6.5; Barnes 6 (Agjei 75, 6), Gray 6.5


Manchester United (4-3-3): De Gea 6; Young 6.5, Bailly 7.5, Blind 6.5, Darmian 6.5; Herrera 7, Fellaini 6.5, Pogba 7 (Carrick 90); Lingard 6 (Rashford 69, 6.5), Martial 8 (Mkhitaryan 79, 6), Rooney 6.5

No comments