Habari

ANTOINE GRIEZMANN KUONGEZA MAKALI YA POGBA MANCHESTER UNITED …dau la pauni mil 85 halizuiliki

on

Ni wazi kuwa safari ya Antoine Griezmann kwenda Manchester United haikwepeki, dau la pauni milioni 85 linalotajwa halizuiliki.
United ipo tayari kuweka mezani pauni milioni 85 ambazo zinatosha kufikia kipengele cha kuununua mkataba wa mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid.

Griezmann mwenyewe amedai hataki kuondoka  Atletico Madrid, lakini wakala wa zamani wa FIFA  Vincent Rodriguez amesema dili la nyota huyo kwenda United ni kama limekamilika. 

“Makubaliano ya pesa kati ya Atlético Madrid and Manchester United juu ya usajili wa Griezmann yameafikiwa,” anaeleza Rodriguez kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Vilabu kadhaa barani Ulaya vikiwemo Paris Saint-Germain, Manchster City, Chelsea na Barcelona vinatajwa kuwania saini ya Griezmann lakini inaaminika timu zote hizo haziko tayari kutoa pauni milioni 85, isipokuwa Manchester United pekee.

Eric Olhats  mshauri wa Griezmann ambaye pia ndiye skauti aliyemvumbua nyota huyo alisema: “Kuna  United, City, Chelsea, Barcelona na Real Madrid ambazo zote zimeonyesha nia ya kumsajili Griezmann na kuna ofa isiyozuilika ya pauni milioni 85”. 
Akizungumza na Kituo cha Telefoot TV cha Ufaransa,  Eric Olhats akafichua kuwa United ilikuwa ya kwanza kubisha hodi na ofa iliyoshiba.

Atletico Madrid iko mazungumzoni na Olhats ili kujaribu kumshawishi Griezmann asiondoke. Wametoa ofa ya maboresho ya maslahi yake na wanataka kuongeza dau la kipengele cha manunuzi.

Pep Guardiola anatajwa kumfanya Griezmann kipaumbele namba 1 kwenye usajili wa kiangazi lakini ana kazi kubwa ya kumzuia mshambuliaji huyo asimfuate swahiba wake mkubwa Paul Pogba ndani ya Old Trafford.

Inaaminika kuwa nyuma ya pazia, Pogba anamshawishi Griezmann kwenda United ili kuendeleza makali yao wanayokuwa nayo kwenye timu ya taifa ya Ufaransa.

Wachambuzi wa soka wanadai iwapo Griezmann atakwenda United, basi watu watarajie kumuona Pogba mpya atakayekuwa na makali yasiyo na mfano katika Premier League.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *