Habari

ANTONIO CONTE ATAMKA MANENO MAZITO JUU YA ZLATAN IBRAHIMOVIC

on

Kocha wa Chelsea Antonio Conte anaamini Zlatan Ibrahimovic amecheza soka la hali ya juu msimu huu ndani ya Manchester United.
Conte ameyasema hayo wakati timu yake ikijiandaa kuikabili Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England utakaochezwa Jumapili.
Conte alipishana na  Ibrahimovic ndani ya  Juventus  – wakati yeye anaacha kuifundisha timu hiyo, Ibrahimovic ndio alikuwa anasajiliwa, lakini alipata wasaa wa kumshuhudia uwanjani kwa miaka mingi nchini Italia. 
Kocha huyo anasema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 yupo katika kilele cha ubora wake akiwa na United chini ya  Jose Mourinho.
“Zlatan yupo katika kiwango bora. Ni mchezaji bora. Sio mmaliziaji tu bali hata kusaidia kuchezesha timu. Ni vizuri kuwa na aina hii ya mchezaji. Kwangu mimi huyu ni mmoja wa wachezaji bora duniani”, anaeleza Conte.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *