Habari

ARSENAL KUMPUNGUZIA MAKALI WENGER KWA KUAJIRI MKURUGENZI WA SOKA …Marc Overmars kipaumbele No.1

on

Kwa mara ya kwanza katika historia yao, Arsenal inataka kuajiri mkurugenzi wa soka, huku mshambuliaji wao wa zamani Marc Overmars (pichani) akitajwa zaidi kushika nafasi hiyo.
Ni hatua ambao inaaminika haitapokewa vema na bosi Arsene Wenger, lakini klabu hiyo inaendelea na mchakato huo bila ya wasiwasi wowote.
Arsenal inamtaka mkurugenzi wa soka ili pamoja na mambo mengine, lakini awe pia  mtendaji mkuu katika nyendo za usajili wa wachezaji. 
Wenger amekuwa mtu pekee mwenye mamlaka ya soka klabuni tangu alipojiunga nayo miaka 21 iliyopita – akiwa na kauli ya mwisho juu ya usajili na mustakabal wa timu.
Overmars ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa soka wa  Ajax, aliitumikia Arsenal kwa miaka mitatu na kushinda mataji ya Premier League na FA Cup chini ya Wenger mwaka 1998.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *