ARSENAL WAPIGWA 3-0 KAMA WAMESIMAMA …wafunikwa na Crystal Palace mwanzo mwisho


ARSENAL wamechapwa 3-0 na  Crystal Palace na kuwafanya Manchester United wasalie nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Washika bunduki hao wa London walifunikwa na Crystal Palace  mwanzo mwisho na kujikuta wanaenda mapumziko wakiwa nyuma 1-0 kwa bao lililofungwa na Andros Townsend kunako dakika ya 17.

Kiungo wa zamani wa Newcastle na PSG, Yohan Cabaye akaifungia Crystal Palace goli la pili dakika ya 63 huku Luka Milivojevic akisukumiza bao tatu kwa mkwaju wa penalti dakika ya 68.


Kwa matokeo hayo, Arsenal inabakia nafasi ya sita na pointi zake 54 huku United ikitesa nafasi ya tano na pointi 57. Timu zote hizo mbili zimecheza michezo 30.

Crystal Palace: Hennessey, Ward, Kelly, Sakho, Schlupp, Milivojevic, Cabaye, Zaha, Puncheon, Townsend, Christian Benteke. 

Arsenal: Martinez, Bellerin, Mustafi, Gabriel, Monreal, Xhaka, Elneny, Walcott, Ozil, Welbeck, Sanchez. 
Mabango ya "Ondoka Wenger" hayakukosekana uwanjani
Toka Wenger, tokaaa!

Msimamo wa Ligi ulivyo

No comments