Arsenal imekubali kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa watani zao wa London, Tottenham kwenye mchezo muhimu wa Premier League.

Matokeo hayo yamekuwa faida kwa Tottenham ambayo inazidi kuipumulia Chelsea kwa tofauti ya pointi nne, lakini kwa Arsenal ni majanga.
Arsenal inaendelea kubaki nafasi ya sita na kuzidi kudidimiza matumaini yao ya kumaliza katika ‘top four’.

Jahazi la Arsenal lilizamishwa kwa mabao ya haraka haraka kutoka kwa Dele Alli dakika ya 56 na Harry Kane aliyefunga kwa penalti dakika ya 58.

Kwa ushindi huo, Tottenham imejihakikishia kumaliza juu ya Arsenal kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995.

Tottenham Hotspur (4-2-3-1): Lloris; Trippier (Walker 88), Alderweireld, Vertonghen, Davies; Dier, Wanyama; Son (Dembele 79), Eriksen, Dele (Sissoko 90+1); Kane

Arsenal (3-4-2-1): Cech; Gabriel (Bellerin 75), Koscielny, Monreal; Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Xhaka (Welbeck 65), Gibbs; Ozil, Sanchez; Giroud (Walcott 81).
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac