ARSENAL YAUA 3-0 NA KUIREJESHA MAN UNITED NAFASI YA SITA


Hatimaye Manchester United imerejeshwa ‘eneo lake la kujidai’ – nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya Englad baada ya Arsenal kuinyuka West Ham 3-0.

Arsenal sasa imefikisha pointi 54 sawa na Manchester United, lakini washika bundiki hao wa London wanajivunia wastani mzuri wa magoli.

Mesut Ozil alikuwa wa kwanza kuifunguia Arsenal dakika ya 58 huku Theo Walcott akifunga la pili dakika kumi baadae kabla ya Olivier Giroud hajashindilia la tatu dakika ya 83.

No comments