Habari

ARSENE WENGER MAMBO MAZITO ARSENAL … ‘hakuna mkataba mpya’

on

Hakika kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anapita katika kipindi kigumu kuliko chochote kile alichowahi kukutana nacho ndani ya maisha yake kwenye klabu hiyo ya London.
Kuelekea mchezo wa watani wajadi dhidi ya Tottenham Jumapili hii, jana usiku mashabiki wa Arsenal wakaweka tangazo kubwa kwenye uwanja wa Emirates kupitia ‘projetor’ ambalo lilisomela Wenger Out (Ondoka Wenger).
Picha za tangazo hilo zikasambaa kwa kasi kwenye mtandao wa Twitter huku baaadhi ya maoni yakisema ‘hakuna mkataba mpya’. 
Mkataba wa Wenger unaisha mwishoni mwa msimu huu lakini mwenyewe amekuwa akisisitiza kuwa ataamua hatma yake pindi msimu utakapomalizika.
Mashabiki hao wa Arsenal hawakushia Emirates peke yake, bali tangazo kama hilo lilionekana pia kwenye uwanja wao wa zamani  Highbury. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *