ARSENE WENGER: SIKU MOJA NITAONDOKA ARSENAL

Arsene Wenger amesema siku moja ataondoka Arsenal lakini bado klabu hiyo itandelea kusalia na ukubwa wake na heshima yake.
Mkataba wa Wenger mwenye umri wa miaka 67 unamalizika mwishoni mwa msimu lakini bado hajaweka wazi iwapo ataendelea kuiona timu hiyo licha ya kuwekewa mezani ofa ya miaka miwili
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakitofautiana dhidi ya meneja huyo katika miezi ya karibuni, wengine wakitaka atimke na wengine wakitaka abakie.
"Siku moja bila shaka nitaondoka, lakini la muhimu ni kwamba Arsenal itasalia kuwa klabu kubwa ambayo inaenziwa na kila mtu”, alisema Wenger.

No comments