AWADH JUMA WA MWADUI UNITED AFAGILIA UWEZO WA "ALIYEMPORA" NAMBA SIMBA SC

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Mwadui United, Awadh Juma amesema kuwa amekoshwa na uwezo wa Said Ndemia ambaye anaitumikia klabu yake ya zamani ya Simba.

Awadh aliamua kuvunja mkataba wa kuitumikia Simba baada ya kuenguliwa kwenye kikosi cha kwanza na kocha mpya, Joseph Omog raia wa Cameroon ambaye anaonekana kuwa na imani na Said Ndemia kwenye kikosi cha kwanza.

“Niliamua kuvunja mkataba wangu na Simba baada ya kuona sipati nafasi ya kucheza mara kwa mara, hivyo sikuwa na namna zaidi ya kushinikiza kuondoka,” alisema Awadh.

“Mwadui ni sehemu salama zaidi kwangu kwa sababu nafikiri nitapata muda mwingi wa kucheza kuliko ilivyokuwa Simba,” aliongeza nyota huyo anayefahamika pia kwa jina la “Mfalme wa Mtani Jembe.”

“Ndemia anacheza nafasi niliyokuwa naitumikia mimi, nakoshwa na uwezo wake, bila shaka ni miongoni mwa viungo bora kabisa kwa kipindi hiki.”


Awadh aliamua kuondoka Simba kutokana na suala zima la kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza na baada ya ujio wa James Kotei kutoka Ghana hivi sasa inafahamika kuwa amesaini mkataba wa awali na timu ya Mwadui FC ambao ni wa miezi sita.

No comments