BAADA YA ARSENAL KUPATA USHINDI WA KUOKOTA SASA 'TOP FOUR' PAWA PATAMU


Arsenal imezidi kuongeza presha kwenye kinyang'anyiro cha 'top four' ya Premier League baada ya kuifunga Leicester City 1-0.

Washika bunduki hao wa London walilazimika kusubiri hadi dakika ya 86 kuambulia bao la kuokota baada ya mlinzi Robert Huth kujifunga.

Nacho Monreal alipiga krosi ambayo kama isingembabatiza Huth kifuani na kwenda wavuni, basi mpira ule ulikuwa unakwenda nje.
No comments