BAADA YA KUDUNGWA 3-0 NA CRYSTAL PALACE, ARSENE WENGER AKIRI ARSENAL “INAELEKEA KUSIKO”

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema mustakabali wake ndani ya klabu hiyo hauwaathiri wachezaji wake, lakini akakiri kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Crystal Palace kilikuwa ni tatizo kubwa.

Wenger bado hajasaini mkataba mpya baada ya ule wa awali kumalizika mwishoni mwa msimu huu, huku akiwa tayari ameandaliwa mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuwafundisha washika bunduki, japokuwa hajatangaza kama ataendelea ama la.

“Nimesimamia zaidi ya michezo 1,100 kwa Arsenal, ila hatujazoea kupoteza mechi kama hivi. Tunapaswa kuchukua hatua haraka sana na sio kukubali,” alisema Wenger.

Baadhi ya mashabiki waliosafiri na timu walimwambia Wenger anatakiwa kwamba anatakiwa kuondoka klabuni hapo kwakuwa hana jipya tena.

“Naelewa mashabiki wetu hawana furaha tena, na sisi wote kwa ujumla hatuna furaha pia.”

“Ninasikitika jinsi tulivyopoteza mchezo huu. Palace walikuwa na kasi, waliwafunga Chelsea siku zilizopita na wameonyesha wana uwezo wa kufanya vizuri.”

“Tupo kwenye nafasi ngumu na matokeo ya mchezo wa jana hayakutusaidia,” alisema Wenger.

No comments