Habari

BAADA YA KUKOSOLEWA NA MOURINHO HATIMEYE IBRAHIMOVIC ASEMA SASA AMECHOKA

on

Mshambuliaji wa Manchester United anayeongoza kwa kuifungia magoli mengi timu hiyo msimu huu, Zlatan Ibrahimovic amejibu hoja juu ya kiwango chake kukoselewa na kocha Jose Mourinho.
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35, alikuwa kwenye kiwango kibovu Alhamisi iliyopita katika mchezo wa Europa League wa sare ya 1-1 dhidi ya Anderlecht ya Ubelgiji na Mourinho hakusita kukosoa kiwango chake pamoja na washambuliaji wengine baada ya mechi hiyo.
Zlatan Ibrahimovic anasema: “Nadhani kocha alikuwa sahihi. Sikuwa najisikia vizuri kwa maana ya kwamba nilikuwa nimechoka lakini hiki sio kisingizio kwasababu bado nawajibika kufanya vizuri zaidi kuliko nilivyofanya.
“Nilijiuliza peke yangu na hakikuwa kiwango bora. Tumecheza mechi nyingi na nimeshiriki karibu michezo yote.
“Bado tuna mwezi mmoja mbele, tunaendelea kupambana tuna Europa League na mwisho wa siku tuna Premier League. Tunapambana kwaajili hiyo”
Zlatan Ibrahimov  mwenye mabao 28 akakiri kuwa anapambana na uchovu wakati kikosi cha Jose Mourinho kikicheza mchezo wake wa  53 Jumapili hii dhidi ya Chelsea kwenye Premier League.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *