BAKARI SHIME AENDELEA KUIFUA SERENGETI BOYS NCHINI MOROCCO

TIMU ya taifa ya vijana, Serengeti Boys imendelea kujifua nchini Morocco chini ya kocha mzawa Bakari Shime, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuanza kwa michuano ya Afcon nchini Gabon.

Akizungumza kwa njia ya mtandao, kocha wa timu hiyo amesema kwamba analishukuru Shirikizo la soka (TFF) chini ya Jamal Malinzi kwa kuwatafutia kambi nzuri yenye hadhi na utulivu kwa ajili ya kufanya maandalizi.

“Hali ya kambi ni nzuri na tulivu, vijana wanajifua vilivyo, hivyo tunaomba Watanzania wazidi kutuunga mkono, tunaahidi hatutawaangusha tutakwenda kupambana vilivyo nchini Gabon,” alisema kocha huyo.

“Kwa kweli tunaishukuru sana TFF kwa kututafutia kambi nzuri na ya kisasa kwa ajili ya kufanya maandalizi, inatia moyo kuwa hapa,” aliongeza.

“Tukishamaliza kambi hapa tutaelekea nchini Cameroon kwa wiki nzima huko nako tutapata mchezo wa kujipima nguvu kabla ya kutimkia Gabon kwenye michuano yenyewe.”


Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Mataifa Afrika kwa ngazi ya vijana ambapo kipindi cha nyuma iliwahi kupata nafsi hii lakini ikapotea baada ya kubainika kumtumia Nurdin Bakari ambaye alikuwa amezidi umri. 

No comments