BANANA ZORRO AMMIMINIA SIFA MRISHO MPOTO

BOSI wa B Band, Banana Zorro amemmwagia sifa mwanamuziki wa kiharakati, Mrisho Mpoto akisema kuwa ni miongoni mwa wasanii wanaompa raha pale anaposikiliza kazi zake ambazo mara zote hubeba ujumbe mzito kwa jamii.

Akiongea na saluti5, Banana amesema kutokana na kuvutiwa naye, ndio maana amekuwa akipenda kufanya kazi nae akimchukulia pia kama mmoja wa walimu wake wa muziki.


“Unapomzungumzia Mrisho Mpoto, kwangu unakuwa unamzungumzia mtu muhimu zaidi kwangu kimuziki baada ya baba yangu mzazi, Zahir Ally Zorro, navutiwa na aina yake ya uimbaji na namna alivyo tajiri wa “meseji”,” amesema Banana.

No comments