BARCELONA DUKA LIKO WAZI, WALAMBWA 3-0 NA JUVENTUS


Barcelona wameanza vibaya kampeni ya robo fainali ya Champions League baada ya kukubali kichapo kikubwa cha bao 3-0 kutoka kwa Juvetuns.

Kwa mara nyingine tena Barcelona watakuwa na mlima mrefu wa kupanda ili kusonga mbele ambapo watahitaji ushindi wa 4-0 katika mchezo wa marudiano utakaochezwa April 19 kwenye uwanja wao wa nyumbani - Camp Nou.

Paulo Dybala ndiye aliyekuwa mwiba kwa Barcelona  kwa kufunga magoli mawili ya mwanzo dakika ya 7 na 22 huku Giorgio Chiellini akihitimisha ushindi kwa bao la dakika ya 55.

Katika mchezo wa hatua ya 16 bora, Barcelona ilifungwa na 4-0 na PSG katika mchezo wa kwanza, lakini kwenye mchezo wa marudiano ikaibuka na ushindi wa 6-1 na kusonga mbele. Je hadithi itajirudia kwa Juventus?

Juventus (4-2-3-1): Buffon 7, Dani Alves 7, Bonucci 8, Chiellini 8, Alex Sandro 7, Pjanic 8, Khedira 7, Cuadrado 7.5 (Lemina, 73), Dybala 9 (Rincon, 81), Mandzukic 6.5, Higuain 6.5

Barcelona (4-3-3): Ter Stegen 7, Sergi Roberto 6, Pique 6, Umtiti 5, Mathieu 6 (A Gomes, 46, 7), Rakitic 6, Mascherano 6, Iniesta 7, Messi 7.5, Luis Suarez 7, Neymar 6

No comments