BAYERN MUNICH YAICHOKONOA REAL MADRID… yamwitaji Mateo Kovacic ndani ya kikosi chao

TAARIFA za tetesi za usajili za mwishoni mwa juma lililopita zinamtaja nyota wa Real Madrid, Mateo Kovacic kuwa anahitajika ndani ya kikosi cha Bayern Munich.

Kwa mujibu wa Daily Star, imemwelezea Kovacic kama ni mchezaji wa awali aliye katika malengo ya klabu hiyo ya Bundesliga.

Hata hivyo Bayern wanakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vigogo wengine wa soka kutoka barani Ulaya wakiwemo Liverpool, Juventus na Paris Saint-Germain waliomo katika mbio za kuwania saini ya kiungo huyo mkabaji.

Kovacic mwenye umri wa miaka 22, ameelezwa kutoficha mapenzi aliyonayo kutaka kuendelea kuwa katika kiwango cha hali ya juu akiwa katika kikosi cha timu yoyote itakayompa nafasi katika kikosi cha kwanza.


Hata hivyo, Bayern imebainisha mpango wake wa kuanza kumfukizia raia huyo wa Croatia na wamemweka katika rada zake za usajili wa majira ya kiangazi.

No comments