Habari

BEKI WA ZAMANI ENGLAND NA ASTON VILLA UGO EHIOGU AFARIKI GHAFLA

on

Beki wa zamani wa timu ya taifa ya England na Aston Villa Ugo Ehiogu amefariki akiwa na umri wa miaka 44 baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo Alhamisi.
Ehiogu alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa katika kituo cha mazoezi cha klabu ya Tottenham Hotspur.
Taarifa ya Spurs ilsiema Ehiogu alifariki mapema Ijumaa akiwa hospitalini.
Ehiogu, ambaye alikuwa mkufunzi wa timu ya Spurs ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23, alikuwa amechezea timu ya taifa ya England mechi nne na kufunga bao moja.
“Hatuwezi kueleza majonzi na huzuni tuliyo nayo katika klabu hii,” mkuu wa ukufunzi na ustawi wa wachezaji Tottenham John McDermott amesema.
Ehiogu alichezea Atson Villa karibu mechi 200 kati ya 1991 na 2000 kisha akacheza miaka saba Middlesbrough.
Alishinda Kombe la Ligi akiwa na Villa mwaka 1994 na 1996 na pia akiwa na Boro mwaka 2004.
Beki huyo pia alichezea West Brom, Leeds, Rangers na Sheffield United, kabla ya kustaafu 2009.
Alianza kazi ya ukufunzi Tottenham mwaka 2014.
Former Tottenham Under 23 coach Ugo Ehiogu, pictured coaching his team, has died after suffering a heart attackKocha wa zamani wa  Tottenham Under 23  Ugo Ehiogu, pichani kabla ya kifo chake akikochi vijana wake Ehiogu won four caps for England, scoring against Spain in a friendly in 2001Ehiogu  aliichezea England mechi nne na kufunga bao mojaThe former central defender is survived by wife Gemma as well as a son and a daughterEhiogu amecha mke na na mtoto mmoja wa kiume 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *