BELLE 9 ASEMA KIFO CHA BABA YAKE KIMEMWACHA KATIKA WAKATI MGUMU

MSANII Abelinego Damian maarufu kama “Belle 9” amesema kuwa, kifo cha baba yake mzazi, Damian Nyamoga aliyefariki usiku wa kuamkia jana kwa ajali ya pikipiki, kimemwacha katika wakati mgumu zaidi.

Akiongea kwa njia ya simu na saluti5 kutoka mkoani Morogoro, Belle 9 amesema kuwa, mzee Nyamoga alikuwa nguzo na mhimili mkuu kwake kimaisha na hata katika masuala ya muziki aliyokuwa akijihusisha nayo.


“Siko vizuri na sijui hali hii itachukua muda gani hadi kupata nafuu, baba yangu alikuwa ndio kila kitu kwangu kuanzia kwenye familia hadi katika muziki,” amesema Belle 9.

No comments