BEN SERENGO AKIRI BONGOMUVI IMESHUKA… ataja kilichoishusha na dawa ya kuirejeshea makali

MKALI wa filamu za Komedi, Ben Serengo amekiri kushuka kwa fani hiyo na kusema kuwa ufumbuzi pekee ni kwa wasanii husika kujenga umoja na mshikamano wa kweli na kuachana na roho za kwanini.

“Sisi wasanii baadhi yetu tunajiona sana, wakati mwingine mtu anahiyari afe njaa kuliko eti kushiriki filamu ya mtu fulani akiamini tu huyo mtu ataibuka na mafanikio kupitia yeye, tunafeli na kuiangusha sanaa yetu,” amesema Ben.

Ben amesema kuwa ifike wakati wasanii watazame mbele na waige mfano wa wasanii wenzao kutoka katika nchi zilizopiga hatua katika sanaa hiyo ama hata hapa Bongo kwa upande wa fani kama bongofleva.


“Hapa kwetu wasanii wa bongofleva wanapeana shavu lakini sisi roho maya zimetutawala, tena kuna baadhi ya wasanii wanafikia hata kuwaombea wenziwao waporomoke kisanii ili waumbuke na thamani yao ipotee katika jamii,” anasikitika Ben.

No comments