BIMBO AKINTOLA WA NOLLYWOOD ATETEA WANAWAKE KUZAA NJE YA NDOA

BIMBO Akintola ambaye anatamba kwenye ulimwengu wa filamu nchini Nigeria, amesema kuwa haoni shida kwa mwanamke kuzaa nje ya ndoa ikiwa tu anamudu gharama za malezi ya motto.

“Mambo yamebadilika sana hivi sasa na hakuna ajabu yoyote kwa mwanamke kuzaa nje ya ndoa ikiwa tu unaweza kumudu gharama za maisha peke yako, alisema staa huyo.

Achiliambali sisi watu maarufu, kuna wanawake wengi tu wasiokuwa na majina makubwa wamezaa nje ya ndoa na maisha wanayaendesha vizuri bila ya kutegemea msaada kutoka kwa mwanaume.”


Nyota huyo amewataka wanawake nchini Nigeria kubadilisha namna ya kufikiria kwa kuacha kuzaa huku akili zikitegemea kupata kila kitu kutoka kwa wanaume ambao wamezaa nao.

No comments