BORUSSIA DORTMUND ILIVYOWAVUA UBINGWA WA GERMAN CUP BAYERN MUNICH


Borussia Dortmund itakumbana na Eintracht Frankfurt katika fainali ya kombe la mtoano - German Cup (DFB Cup) baada ya kuwalaza wapinzani wao wakubwa Bayern Munich 3 -2 ndani ya dimba la Allianz Arena.

Ousmane Dembele alifunga bao la ushindi na kuipeleka Dortmund fainali ya DFB kwa msimu wa nne mfululizo na kuwatupa nje mabingwa watetezi. 

Marco Reus aliipa Dortmund bao la kuongoza dakika ya 19 lakini Bayern wakachomoa na kuongoza kabla ya mapumziko kupitia magoli ya Javi Martinez na Mats Hummels.  

Pierre-Emerick Aubameyang akaisawazishia Dortmund dakika ya 69 kabla Dembele hajafunga la ushindi dakika ya 74.

No comments