Habari

BRIGHTON YAITANGULIA NEWCASTLE KWENDA PREMIER LEAGUE

on

Brighton imekuwa timu ya kwanza kufanikiwa kupata tiketi kupanda daraja ambapo sasa msimu ujao itacheza Ligi Kuu ya England.
Klabu hiyo imepanda daraja baada ya kuichapa Wigan 2-1 na kufikisha pointi 92 zilizotosha kuwapeleka Premier League huku wakiwa na mechi tatu mkononi.
Newcastle inayowania kurejea Ligi Kuu, iko sehemu nzuri ingawa imekupali kichapo cha bao 3-1 kutoka kwa Ipswich na kuifanya isalie na pointi zake 85, nafasi ya pili kwenye  msimamo wa Ligi Daraja la kwanza (Championship). 
Reading inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 79 wakati Huddersfield Town yenye pointi 78 ipo nafasi ya nne.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *