BUKU TANO TU KUZIONA YANGA, MC ALGER UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI HII

KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika kati ya wenyeji, Yanga na MC Alger ya Algeria kitakuwa ni sh. 5,000.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Taiafa, Dar es Salaam na viingilio vingine vitakuwa ni sh. 20,000 kwa VIP B na C na 30,000 kwa VIP A.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema mandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri.

Mchezo wa kwanza Aprili 8, mwaka huu uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam utachezeshwa na Louis Hakizimana atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Theogene Ndagijimana na Jean Bosco Niyitegeka wote kutoka Rwanda.

Mchezo wa marudiano Aprili 14 nchini Algeria utachezeshwa na marefa wa Guinea ambao ni Yakhouba Keita, Aboubacar Doumbouya na Mamady Tere na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.


Mwaka jana pia Yanga ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikishgo ambako ilifuzu baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola.

No comments