CAF YAAFIKI MECHI YA YANGA NA WAARABU KUPIGWA KIRUMBA

MKAGUZI wa Shirikisho la soka Afrika (CAF), Maxwell Mtonga kutoka Malawi  ameridhia mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga na MC Alger ya Algeria uchezwe uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Aprili 8, mwaka huu baada ya marekebisho madogo aliyoyaelekeza.

Mtonga yupo Mwanza tangu katikati ya wiki akiongozwa na mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF),Salum Madadi katika ukaguzi huo na ameagiza marekebisho madogomadogo

Meneja wa uwanja wa CCM Kirumba, Steven Shijja amesema watahakikisha wanafanya marekebisho hayo ndani ya muda kama walivyoelekezwa na mchezo huo utafanyika Mwanza bila shaka.

Viongozi wa Yanga wapo katika harakati za kufanikisha mpango wa kuuhamishia mchezo huo Mwanza kutoka uwanja wa taifa, Dar es Salaam kwa matarajio ya kupata watazamaji wengi na pato kubwa.

Tayari mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Mbao FC na Simba SC ya Dar es Salaam ulikuwa ufanyike Arili 8 mwaka huu uwanja wa CCM Kirumba, umesogweza mbele kwa siku mbili hadi Arili 10.

Lakini taarifa ya  mkurugenzi wa bodi ya Ligi, Boniphace Wambura  ilisema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha shughuli za kijamii kwenye uwanja huo zitakazoanza Aprili 1 hadi 9.


Yanga SC imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanaco uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka ichini Zambia ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

No comments