CANNAVARO ASEMA WAAlGERIA NI WEPESI TU... adai watawang'oa tu huko kwao

NAHODHA wa Yanga, Nadri Haroub “Cannavaro” amesema safari yao ya kuelekea Algeria itakuwa nyepesi kutokana na ushindi wa bao 1-0 na kwamba hakuna watakachohofia.

Akizungumza na Saluti5, Cannavaro alisema MC Alger hawakuwa tishio lolote kwao na kwamba ilikuwa wapate ushindi mzuri endapo wangetumia nafasi walizopata katika mchezo huo.

Cannavaro alisema kwa sasa wanajipanga katika mchezo wa marudiano ambapo hawana hofu katika mchezo huo kutokana na uzoefu walionao katika mechi dhidi ya Waarabu.

Nahodha huyo alisema watapambana kuwadhibiti waarabu hao katika dakika 20 za kwanza ambazo huwa za kasi ambapo pia watatafuta bao la mapema litakalowachanganya MC Alger.

“Watu wanaweza kuona ushindi tulioupata ni mdogo lakini ukweli ni kwamba huu ni ushindi mzuri kwetu kwa kuwa hatujaruhusu bao lolote nyumbani,” alisema Cannavaro.


“Kwa sasa tuna uzoefu mkubwa na mechi za ugenini, tunajua kila mbinu za huko tunachotaka ni kutulia kuwadhibiti dakika 20 za kwanza lakini pia kama tukipata bao la mapema litawachanganya zaidi wenzetu.”

No comments