CANNAVARO ASIKITIKA KUIKOSA SIMBA NUSU FAINALI YA KOMBE LA FA

BEKI mkongwe wa timu ya Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" amesema kuwa alitamani wapangwe na Simba kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA ili wapate nafasi ya kulipa kisasi na kuhitimisha tambo za wekundu hao wa Msimbazi.

Cannavaro alisema kuwa wanaichukulia mechi hiyo kwa uzito kama ambavyo wanagepangwa na klabu kubwa kama Simba.

“Nilitamani tukumbane na Simba kwenye hatua hii ili kumaliza ubishi, ni mechi yenye msisimko mkubwa nchini lakini hakuna namna mchezo wetu na Mbao tutauchukulia kwa ukubwa ule ule,”alisema beki huyo mkongwe.

“Nia yetu ni kuona Yanga inashiriki tena kwenye michuano ya kimataifa kwa kutwaa mataji yote kama tulivyofanya msimu uliopita,” aliongeza beki huyo ambaye amekaa nje ya kikosi kwa muda mrefu sababu ya majeruhi.


Baada ya Simba kupokwa pointi zake tatu, Yanga imekuwa na njia nyeupe ya kubeba makombe yote mawili ikiwa tu watashinda katika mechi zote ambazo zinafuata kwenye Kombe la FA na michuano ya Ligi Kuu Bara.

No comments