CANNAVARO ATETA MAZITO NA MANJI KUHUSU "MUSTAKABALI" WA WACHEZAJI YANGA

NAHODHA wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro amepiagia simu mwenyekiti wa timu hiyo Yussuf Manji na kuteta mazito akimwambia atulie kila kitu kinafanyiwa kazi kwa utulivu na kwa akili kubwa.

Naodha huyo aliyerudi katika utumishi wa nafasi yake katika safu ya ulinzi ya Yanga, alilazimika kumpigia simu bilionea huyo na kuteta nae kutokana na ukimya wake tangu atoke katika matatizo yake.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba katika mazungumzo yao, Cannavaro ametakiwa kuwa mtulivu na kuwakumbusha wenzake kuwa Manji bado yuko Yanga na kwamba kinachoendelea sasa ni kuweka sawa mambo yake binafsi kwa kuwa wakati wote alikuwa katika matatizo yaliyomkuta.

Chanzo hicho cha kuaminika kimeiambia Saluti5 kuwa mbali na hivyo, Cannavaro amehakikishiwa kwamba madai yao yete yanajulikana na yatafanyiwakazi haraka mara baada ya kuanza kuzifanyia kazi changamoto za klabu hiyo.

“Unajua baada ya Sintomfahamu hii Cannavaro alimpigia simu Manji na kuzungumza nae katika kupeleka kilio chao na mwenyekiti alimsikiliza na kumtaka atulie kwani anafanyia kazi yote aliyomletea,” kilisema chanzo hicho.


“Amemwambia mengi lakini kubwa ni kwamba amemweleza yeye hajaamua kuondoka Yanga na kwamba kuna mambo anayaweka sawa katika makampuni yake akimaliza atarudi katika utendaji wake na akaongezea kwamba anafuatilia kwa karibu kila kitu kinachoendelea.”

No comments