CANNAVARO AWATAKA SIMBA WASIOJIDANGANYE KUHUSU UBINGWA WA LIGI KUU WA VODACOM

Baada ya yanga kutolewa kwenye michuano ya shirikisho,  nahodha wa kikosi cha Yanga, Nadir Haroub Cannavaro amesema kwamba mapambano yao yote sasa wanayaelekeza kwenye kutetea ubingwa wao wa ligi ya voda.

Cannavaro amesema kuwa bado ni mapema kuipa Samba ubingwa kwa sababu hata wao wanawinda ubingwa huo kimya kimya.

“Simba wasijidanganye hatua yao ya kuongoza ligi mpaka sasa hivi sio kubeba ubingwa wa Ligi Kuu, tupo makini na hesabu zetu za ubingwa bado ziko palepole,” alisema beki huyo kisiki.

“Hatuwatazami wao kama wanavyodhani, tunacheza mechi na kuhakikisha tunashinda, bado mda upo lolote linaweza kutokea kwa sababu bado hakuna pengo kubwa kati yetu,” aliongeza Cannavaro.


Beki huyo alikosekana uwanjani kutokana na kuwa majeruhi lakini hivi sasa yupo fiti na kocha ameanza kumpa mechi za kucheza kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uzoefu aliokuwa nao. 

No comments