CARLO ANCELOTTI AMRUKA GARETH BALE FUTI MIA BAYERN MUNICH

CARLO Ancelotti ametolea nje majadiliano ya kuungana tena na mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale, huku bosi huyo wa Bayern Munich akidai kuwa uvumi huo wa uhamisho ni “hadithi”.

Carlo Ancelotti alimnunua Gareth Bale kutoka Tottenham Hotspur kwenda Real Madrid mwaka 2013 kwa ada ya rekodi ya dunia ya pauni mil 85.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales hivi karibuni alishinda majeraha ya kifundo cha mguu yaliyokuwa yakimkabili Bernabeu.

Rekodi ya nyota huyo ya pauni mil 85 ilivunjwa na Paul Pogba msimu uliopita akisajiliwa kwa pauni mil 89 na Manchester United akitokea Juventus.


Bale amekuwa na msaada mkubwa kwa “Los Blancos” kwenye safu ya ushambuliaji akishirikiana na Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.

No comments