Timu ya K.R.C. Genk ya Ugiriki anayokipiga Mbwana Samatta wa Tanzania, imeshindwa kuvuzu hatua ya nusu fainali ya Europa League baada kutolewa na Celta Vigo ya Hispania kwa jumla ya bao 4-3.

Genk imeambulia sare ya 1-1, matokeo ambayo hayajatosha kuwapa tiketi ya nusu fainali. Katika mchezo wa kwanza Celta Vigo walishinda 3-2.

Cetla Vigo walifunga bao lao dakika ya 65 mfungaji akiwa Pione Sisto na kudumu kwa dakika nne tu kabla Leandro Trossard hajaisawazishia Genk.

Timu zingine zilizosonga mbele ni Ajax iliyoing’oa Schalke 04 na Lyon iliyoitoa kwa matuta Besiktas.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac