RAPA Drake alilazimika kuivunja shoo yake mjini Amsterdam Jumatatu hii baada ya kudaiwa kuugua ghafla, kumbe rapa huyo alikula chakula chenye sumu!

Mtu wa karibu wa rapa huyo ameuambia mtandao wa TMZ kuwa rapa huyo alikula chakula hicho chenye sumu muda mfupi kabla ya kufanyika kwa shoo hiyo.

Drake alikimbizwa hospitali ndipo madaktari walipomshauri kutofanya shoo hiyo. Mashabiki walimsubiri rapa huyo katika ukumbi wa Ziggo Dome kwa ajili ya kutumbuiza kwa muda wa dakika 75 kabla ya kutangazwa kuvunjika kwa shoo hiyo.

Hata hivyo shoo hiyo inatarajiwa kufanyika tena Jumatano hii katika ukumbi huo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac