CHARLES BONIFACE MKWASA ATULIZA PRESHA YANGA SC

BAADA ya kuwepo kwa fununu za mgomo ndani ya kikosi cha Yanga, Katibu mkuu wa kikosi hicho, Charles Boniface Mkwasa ameweka wazi mipango ya fedha ambayo inafanywa na uongozi ili kuweka sawa hali ya mambo.

Katibu mkuu huyo amewataka wachezaji kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho klabu inakusanya fedha kwa nguvu zote ili kulipa malimbikizo  yote yaliyokuwepo kipindi cha nyuma.

“Ni kweli zipo taarifa nyingi ambazo zilienea lakini niwatoe hofu tu kuwa kila kitu kinakwenda sawa na hivi sasa uongozi upo makini kukusanya fedha kwa ajili ya kuendesha timu,” alisema Katibu huyo.

“Yapo mambo mengi yanafanyika hivi sasa ikiwemo kukusanya michango ya wanachama pamoja na madai yetu ya fedha za matangazo ya Terevisheni,” aliongeza Mkwasa ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa.


Yanga inatarajia kurudiana na MC Alger wiki hii nchini Algeria katika mchezo wa Kombe la CAF huku ikiwa na kibarua kigumu cha kutetea ubingwa wa Ligi Kuu. 

No comments