CHEGGE ASEMA MASHABIKI HAWAJAELEWA MAANA YA WIMBO WAKE MPYA WA "GO DOWN"

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Chege Chigunda amesema kuwa watu bado hawajauelewa wimbo wake mpya wa "Go Down" ambao ameufanya na rafiki yake mkubwa, Mheshimiwa Temba.

Chege alisema kuwa licha ya watu wengi kuvutiwa na wimbo huo, lakini bado mashabiki wake wanaonekana kutouelewa vizuri ujumbe wake.

“Ni wimbo wangu na Temba ambao unaoihusu jamii moja kwa moja na wala hauhusiani na upepo wa siasa na hauna lengo la kumzungumzia mtu yeyote,” alisema Chege.
“Ni ngoma ambayo inahusu wale watu wote wenye hulka ya kuwa na maneno mengi lakini hatujagusa mtu wala itikadi yoyote ya kisiasa,” aliongeza Chege.

Tangu kuvunjika kwa kundi la TMK Wanaume, Chege na Temba wameendelea kufanya kazi pamoja kama timu na kuteka soko la muziki wa kizazi kipya.

No comments