CHRISTIAN BELLA NA MALAIKA BAND KUKINUKISHA MPO AFRIKA TANDIKA USIKU HUU

MALAIKA Music Band chini ya Christian Bella “King Of The Best Melodies” wanatarajiwa kuutumia mkesha wa Jumapili ya Pasaka kwa kumwaga burudani kabambe ndani ya Mpo Afrika, Tandika Davis Corner, jijini Dar es Salaam.

Shoo hiyo iliyopangwa kuanza kuunguruma majira ya saa 3:30 usiku, inatazamiwa kujaa msisimko wa hali ya juu, hasa kwa kuwa Bella anayetikisa vilivyo anga la muziki wa dansi, ana muda mrefu hajatua maeneo hayo kumwaga raha.


Baadhi ya mashabiki pamoja na wapenzi mbalimbali wa muziki wa dansi wameonekana kuonyesha kuisubiri kwa hamu shoo hiyo itakayoambatana na utambulisho wa vibao vipya vya mkali huyo wa sauti Bongo kwa upande wa dansi.

No comments