Habari

CRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI MPYA YA MAGOLI 100 ULAYA

on

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 100 kwenye michuano ya Ulaya kwa ngazi za klabu, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa.
Mshindi huyo wa mara nne wa tuzo yaBallon d’Or  hakufunga kwenye mechi sita zilizopita za Champions Lague, lakini safari hii akaibuka shujaa baada ya kuitoa nyuma 1-0 timu yake na kuibuka na ushindi.
Ronaldo amefikisha magoli hayo 100 kupitia timu mbili – Manchester United na Real Madrid ambapo bao lake la kwanza lilikuja mwaka 2007 wakati United ilipoichapa Debrecen 3-0.

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *