DAVIDO AKANUSHA KUSHIRIKI VIDEO YA NGONO ILIYOTAPAKAA MITANDAONI

STAA wa muziki nchini Nigeria, Davido amekanusha kushiriki kwenye video ya ngono ambayo ilirushwa mtandaoni hivi karibuni na kupata watazamaji 6000.

Katika video hiyo, kunaonekana picha ya mtu mwenye muonekano kama yake, hali iliyosababisha taharuki kwa mashabiki wa staa huyo.

Davido ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya shoo, amekanusha vikali kuhusika kwa lolote kwenye video hiyo.

“Sihusiki na lolote juu ya video hiyo na wala sijawahi kuwa na mpango wa kufanya jambo kama hilo kwenye maisha yangu,” alisema Davido.


“Naheshimu hisia za mashabiki wangu na daima siwezi kuyaweka hadharani masuala yangu binafsi,” aliongeza nyota huyo anayefanya vyema kwenye tasnia ya muziki.

No comments